Wednesday, 30 January 2019

Kambini Kichokochwe watoa neno kwa NGENARECO na Direct AID

Imeandikwa na Asha Haji , Pemba
Wananchi wa kijiji cha Kambini kwajuni Shehia ya kambini kichokochwe  Wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba wamesema, wanajisikia faraja kufikiwa na huduma ya maji safi na salama kwani muda mrefu waliishi pasi na kuwepo huduma hiyo.
Aidha wamelishuhukuru shirika na DIRICT AID (Africa Muslim Agency) kwa kujitolewa kuwachimbia kisima kijijini  kwao wakisema kuwa kufanya hivyo kuna dhihirisha kuwa taasisi hiyo ina mapenzi ya dhati kwa wananchi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika kijiji kwao walisema, waliishi na dhiki kwa muda mrefu huku wakilazimika kwenda masafa marefu kufuata huduma hiyo lakini walisema , ingawa bado changamoto hiyo ipo lakini kwa kiasi fulani imetatuka baada ya kutokea wafadhili kuwajengea kisima hatimae wameanza kuneemeka.
Asha Mwinyi Hamad mmoja miongoni wanakijiji hicho alisema muda mrefu waliamua kupambana na hali hiyo hadi pale mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar PAZA (Promoting Accountability of Zanzibar)ulipo wafikia kijijini mwao.
Alisema mradi huo ulikua na uhamasishaji mkubwa kwa wananchi juu ya kupigia mbio haki zao ikiwamo hiyo huduma ya maji  , hivyo wananchi waliamua kuyafanyia kazi mafunzo hayo kwa kudai haki yao ya kupata huduma ya maji hatimae walifika hadi kwa wafadhili na kuwachimbia kisima.
Nae Siti Hamad Rashid alisema, wanawashukuru sana NGENARECO  na wadau wenzao kuwaletea mradi huo kwani umewafanya wawe na uwezo wa kuzungumzia haki zao popote pale kwa mujibu wa sharia.
“lakini ingawa kisima kipo lakini hakitoshelezi kutokana na watu waliyopo, bado tunawaomba wahusika watufikirie, lakini tunashukuru kwa hapa tulipopata”alisema Siti.
Kwa upande wake Bakari Suleiman Juma ambae ni mwezeshaji wa wananchi kupitia mradi wa PAZA alisema, tokea wananchi kufikiwa na mradi huo kwa kiwango kikubwa wameamka kufuatilia haki zao kiasi ambacho mpaka walifika katika shirika la DIRECT AID  na kuamua kuchimbiwa kisima.
Mwananchi wa kijiji cha Kambini akionyesha kisima walichochimbiwa na akitoa maelezo jinsi mradi wa PAZA ulivyo wanufaisha
Akielezea zaidi alisema, anatamani kuona mradi unaendelea ili wananchi wazidi kunufaika kwa kupata taaluma ya kujielewa katika kufuatilia haki zao
“kwakweli mradi umesaidia sana, wananchi wanaonekana kabisa wamenufaika” alisema mwezeshaji huyo.
Mradi huo umekuja kwa lengo la kukuza uwajibikaji katika majukumu hatimae kufikia mendeleao katika eneo husika na unaendeshwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania –TAMWA upande wa Zanzibar , Jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar – WAHAMAZA na NGENARECO – PEMBA chini ya mradi wa kuziwezesha asasi za kiraia Zanzibar, ZANSASP,ambapo mradio huo upo ikingono kumalizika na unatarajiwa mwezi wa Pili mwaka 2019

Kundi la wahamiaji haramu wanaswa ziwa tanganyika

Idara ya uhamiaji mkoani Rukwa imewakamata wahamiaji haramu 71 katika operesheni inayoendelea kwenye tarafa ya Wampembe, katika mwambao wa ziwa Tanganyika ambaowahamiaji hao wanasadikiwa kuwa ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afisa Uhamiaji wa Rukwa, Naibu Kamishna Elizeus Mushongi amesema tayari wamewarejesha nchini DR Congo wahamiaji 14, huku wengine wakiwa na hali mbaya kiafya.

Serikali yacharukwa mauaji ya watoto Njombe, yaahidi kuwashika Wahusika

Wabunge wasimama kidete kupinga matukio ya kikatili yanayoendelea kutokea mkoani Njombe ambapo watoto wamekuwa wakiuawa kikatili na baadhi kunyofolewa sehemu zao za siri.


Akizungumza wakati akijibu swali Bungeni, Waziri wa mambo ya ndani Mh. Kangi Lugola,  amesema kwamba tukio hilo kweli limeleta taharuki kwa wakazi wa Njombe, lakini jeshi la polisi limeshachukua hatua kuweza kulikabili.
Akiendelea kufafanua zaidi Waziri Lugola amesema kwamba hivi sasa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni yuko mkoani Njombe kufanya vikao na kamati za ulinzi na usalama,  kutafuta na kuwachukulia hatua wale waliohusika kufanya matukio hayo ya mauaji kwa watoto wasio na hatia.
“Ni kweli kumekuwa na sintofahamu na taharuki katika mkoa wa Njombe kutokana na vitendo vya baadhi ya watanzania wenzetu, wamekuwa wakichukua watoto wadogo na kuwaua, kuanzia juzi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni yuko Njombe, anafanya vikao na kamati za usalama za Wilaya na Mkoa kuhakikisha kwamba vitendo hivi vinakomeshwa, lakini taarifa za awali zinaonesha ni imani za kishirikina”, amesema Waziri Lugola.
Waziri Lugola ameendelea kwa kuwataka wabunge kutoa ushirikiano juu ya suala hilo, na kuwapa onyo Watanzania wote kuacha vitendo hivyo vya kikatili.
Wabunge watupe ushirikiano kwa sababu maeneo yale wanayafahamu vizuri, nitoe onyo kwa Watanzania wote, wasitingishe kiberiti cha serikali ya Rais Magufuli, wasipoacha vitendo hivyo watakipata cha mtemakuni, na tumeshaanza na kule Njombe”, ameongeza Waziri Lugola.
Hivi karibuni kumetokea mauji ya kutisha mkoani Njombe, ambapo watoto wamekuwa wakiuawa kikatili na baadhi kunyofolewa sehemu za siri.

SMZ imara katika kuimarisha Rasilimali za bahari

Naibu waziri wa kilimo Maliasili,Mifugo na Uvuvi Dk.Makame Ali Ussi akizungumza katika mafunzo ya siku tatu kwa wafugaji wa Samaki na watendaji wa sekta za mazao ya Bahari juu ya ufugaji wa Mazao ya baharini katika ukumbi wa kituo cha kuzalishia vifaranga vya mazao ya bahari Bet al ras Bububu wilaya ya Magharib A Unguja amesema serekali inatambua umuhimu wa rasilimali za bahari ambazo zinachangia kuengeza mapato ya nchi pamoja na kuwawezesha wananchi kujikwamua na umaskini.
Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea na jitihada mbalimbali katika kutatua matatizo yanayowakabili wavuvi na wafugaji wa mazao ya bahari ikiwemo Majongoo,Samaki na Kaa.
Dk.Makame amesema wakati umefika kwa Sekta ya bahari kuendelea kuwa muhimili mkuu utakaochangia ukuwaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa chakula.
Amesema takwimu za uzalishaji wa mazao ya baharini zinaonesha kuwa takribani asilimia 40 inawawezesha wananchi kunufaika na ajira ambapo asilimia 70 ya wananchi wanategemea sekta hiyo katika kujikwamua na umaskini jambo linachangia ukuwaji wa maendeleo nchini.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia mifugo na uvuvi Dk.Islam Seif amesema ili kuhakikisha Wavuvi na wafugaji wanafikia malengo waliyoyakusudia Wiizara itaendelea kushirikiana na wataalamu katika kutatua matatizo yanayojitokeza katika sekta hiyo.
Amesema mpaka sasa muitikio kwa wafugaji umekuwa mkubwa ambapo hadi kufikia Wavuvi 49 elfu kutoka 35 elfu jambo ambalo linachangia maendeleo ya Uchumi Nchini.
Ametowa wito kwa Wavuvi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wa maendeleo katika kuleta maendeleo pamoja na kuwa na matumizi mazuri rasilimali za bahari ili ziweze kuwanufaisha wananchi.
Mratibu wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya Samaki Bet al ras Buriani Mussa amesema ni vyema kwa wananchi hususan vijana kuchangamkia fursa zilizopo za kujikita na ufugaji wa mazao ya baharini ili waweze kujingizia kipato cha uhakika.
Amesema si vyema kwa vijana kushindwa kushiriki katika miradi inayoanzishwa badala yake watafute njia mbada za kuweza kujiajiri na kuachana na mawazo ya kusubiri ajira kutoka serikalini.
Washiriki wa mafunzo hayo Naima Ibrahim na Semen Muhammed wameomba kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kuzalisha mazao ya bahari yanayoendana na mahitaji ndani na nnje ya nchi.
Wamesema mbali na mafunzo pia ni vyema kwa wasimamizi wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya mazao ya bahari kufanya kazi kwa uhakika ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia ikiwemo kuondoa tatizo la upatikanaji wa vifaranga kwa wafugaji.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kudumu kwa siku tatu kwa lengo la kuwafunza wafugaji na wasimamizi wa mazao ya baharini namna bora ya kuimarisha ufugaji wa mazao hayo umekutanisha pamoja Wafugaji ,Wataalamu wa Masuala ya Bahari na Watendaji wa Wizara ya kilimo chini ya ufadhili wa FAO na KOICA pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wajasiriamali Zanzibar washauriwa kutumia mitandao kutangaza bidhaa zao

Wajasiriamali nchini wametakiwa kutumia Vyema Miradi ya Maendeleo inayoanzishwa na taasisi mbali mbali ili waweze kunufaika na Bidhaa zao wanazodhalisha.
Akisoma ripoti fupi kwa waandishi wa habari juu ya Utekelezaji wa Mradi wa kukuza ushirika juu ya asasi za kiraia katika midahalo ya sera na Maendeleo  katika ukumbi wa ofisi ANGOZA Mombasa Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwamvuli wa asasi za kiraia ANGOZA Hassan khamis Juma amesema Mradi huo umeelekeza nguvu zao kwa wananchi hususani Wajasiriamali ili waweze kujikwamua na ugumu wa maisha.
Amesema mpaka sasa tayari wamesha anza kutoa Elimu mbalimbali juu ya upatikanaji wa soko kwa bidhaa wanazodhalisha wajasiriamali kupitia mitandao ya kijamii.
Amesema  ili mradi huo uweze kufikia malengo yaliyokusudiwa  ni vyema kwa Wajasiria mali kutumia vyema soko la wazi kupitia Mitandao ya kijamii ili waweze kuendana na ukuwaji wa sayansi na Teknolojia katika kuimarisha maendeleo ya Nchi.
Amesema mbali na Mradi huo kujikita katika kuwatafutia soko Wajasiriamali lakini pia Wamejikita katika kukuza uelewa kwa wananchi juu ya nishati mbadala pamoja na kuandaa kongamano la mwaka linalotarajiwa kufanyika febuari 26-27 mwaka huu ambalo litakutanisha pamoja asasi mbalimbali za kiraia zilizopo Nchini.
Akizungumzia suala la utumiaji Nishati mbadala ambayo pia inatekelezwa na mradi huo Mkurugenzi Hassan amesema jumla ya Wanachama 60 unguja na Pemba wameshapatiwa Elimu ya Nishati mbadala na tayari imeanza kuwanufaisha.
Amesema elimu hiyo imewasaidia kuepukana na gharama za matumizi ya umeme ya kawaida ambayo baadhi ya wananchi wa kipato cha chini wanashindwa kumudu gharama hizo.
Kwa upande wake Afisa Tehema kutoka Angoza Issa Mbwana amesema licha ya elimu iliyotolewa juu ya kutumia Mitandao ya kijamii kwa wajasiriamali bado mwamko umekuwa mdogo ambapo jumla ya wajasiriamali  41 waliopatiwa mafunzo 22 pekee ndio wanaoendelea kutumia mitandao kutangaza bidhaa zao.
Aidha amesema wataendelea kushirikiana na wajasiriamali mbalimbali katika kukuza bidhaa zao hususan katika masuala ya Vifungashio ,ubora na jinsi ya kupata masoko kupitia mitandao ya kijamii.
Mradi huo wa kukuza ushirika wa asasi za kiraia katika Midahalo ya kisera na maendeleo umekusudiwa kutekelezwa katika kipindi cha Miezi 11 ambapo umeanza juni 2018 na unatarajiwa kumalizika April2019 chini ya ufadhili wa Jumuiya ya ulaya EU.    

Rais Magufuli amteua aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa kilimo Zanzibar kuwa Mkurugenzi Mkuu DSFA

Rais Dkt John Pombe Magufuli leo Januari 30 amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi- Zanzibar Dkt. Islam Seif Salum kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).

Tuesday, 29 January 2019

Idadi ya waliokufa kwa kula chakula chenye sumu yaongezeka Pemba



Idadi ya waliokufa kutokana na kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Shanake Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni, imeongezeka na kufikia sita baada ya mmoja miongoni mwa waliyokuwa wakipatiwa matibabu hospitali kufariki dunia siku ya Jumamosi.
Akizungumza Daktari wa zamu katika hospitali waliyolazwa ya Micheweni Dkt. Hamad Said Hamad, amemtaja mwengine aliyefariki ni
Chumu Sadiki Shoka (28) na kusema bado wagonjwa wengine wanne wanaendelea na matibabu.
Aliwataja wagonjwa hao kuwa ni  Asma Makame Ali (12), Rashid Sadi Khatib (10), Shajiya Kombo Shoka (25) na Chumu Shiba Faki, anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 35.
“Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wanapatiwa matibabu alifariki jana (juzi) ambapo kwa sasa tunaendelea kuwatibu wagonjwa wanne, ambao hali zao zinaendelea vizuri, isipokuwa Asma Makame Ali, hali yake sio nzuri sana,” alisema.
Wengine waliofariki dunia kutoka na tukio hilo, ni Hafidh Khatib Rashid, Hifidh Khatib Rashid ambao ni watoto mapacha, Fatma Khatib Ali, Sabra Said Rashid na Hamida Bakar Rashid.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kwamba kwa kuwa waathirika hawajawa tayari kutaja aina ya chakula walichokula, ni vyema serikali kuharakisha uchunguzi.
Katika maelezo yao waathirika wa tukio wametofautiana kuhusu chakula walichokula, ambapo baadhi wanadai kwamba walikula dagaa,  wengine samaki aina ya  ngogo na kasa na baadhi yao walisema walikuwa wali kwa maharage.
Hivyo chakula kilichopelekea tatizo hilo bado hakijafahamika.

CAF yasogeza mbele mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamua kusogeza mbele kwa wiki moja kuanza kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika 2019, kutoka Juni 14 hadi Juni 21 kwa sababu ya kupisha mfungo wa radamani.
Makamu wa rais wa Shirikisho la Soka la Misri (EFA), Ahmed Shobir alitangaza kuwa CAF wamefikia uamuzi huo baada ya kupata maombi kutoka nchi mbalimbali.
“Nchi za Afrika Kaskazini zimeomba CAF kusongeza mbele kwa wiki moja kufanyika kwa mashindano hayo ili kutoa nafasi ya kumalizika mfungo wa Ramadan pamoja na kusherekea siku kuu ya Eid Al-Fitr,” alisema Shobir.
“CAF imekubaliana na nchi kuhusu kusogeza mbele tarehe ya kuanza mashindano kuwa Juni 21 badala ya Juni 14, hivyo mashindano haya yatafikia mwisho Julai 19, 2019,” aliongeza Shobir.
Novemba, CAF ilipoka wenyeji Cameroon kutokana na kuchelewa kukamilisha maandalizi ya miji yake kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 24.
Misri wamechukua wenyeji wa AFCON baada ya  Morocco iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kuchukua wenyeji huo, lakini dakika za mwisho walijitoa.
Misri ilipata kura 16 kati 18 zilizopigwa na wajumbe wa CAF, huku kura moja ikienda kwa Afrika Kusini katika mchakato wa kupata mwenyeji mpya.
Hii ni mara ya tano kwa Misri kuwa wenyeji wa AFCON baada ya kufanya hivyo 1959, 1974, 1986 na 2006, huku Mafarao hao wakishinda mara tatu kati ya mara nne walizokuwa wenyeji.

Wananchi wachoma kanisa wakidai linaleta pepo wachafu

Wananchi wenye hasira kali wamevamia katika eneo la Kanyogoga Wilaya ya Gulu nchini Uganda na kuchoma Kanisa moja muda mfupi baada ya ibada ya asubuhi, kwa madai kuwa linawaletea pepo wachafu.
Wakaazi wa eneo hilo lililoko Kaskazini mwa nchi hiyo wameeleza kuwa wamekuwa wakichukizwa na mienendo ya ibada ya Kanisa hilo linalofahamika kama ‘Jesus is the Living Stone’ ambayo ni kinyume cha mafundisho ya Kikristo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Kanisa hilo lilikuwa limefungwa na Serikali lakini mchungaji wake alikaidi amri hiyo halali.

Monday, 28 January 2019

Facebook kuunganisha WhatsApp, Instagram na Messenger

Chapa ya Facebook

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMpango huo utawaruhusu wateja kuwasiliana kupitia huduma tofauti.
Facebook ina mipango ya kuunganisha huduma zake za kutuma ujumbe katika Instagram, WhatsApp na Facebook Messenger.
Licha ya kwamba huduma zote tatu zitasalia kuwa programu huru zitashirikiana kupitia ujumbe utakaotumwa kutoka huduma moja hadi nyingine.
Facebook imeambia BBC kwamba ndio mwanzo wa mchakato mrefu.
Mpango huo kwanza uliripotiwa mjini New York na unaaminika kuwa mradi wa kibinafsi wa mwanzilishi wa facebook Mark Zuckerberg.
Utakapokamilika , ushirikiano huo utamaanisha kwamba mtumiaji wa facebook anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtu ambaye anamiliki akaunti ya WhatsApp.
Hili haliwezekani kwa sasa kwa kuwa programu zilizopo hazina uhusiano.
Hatua ya kuunganisha huduma hizo tatu umeanza , kulingana na gazeti la The new York Times na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019 ama mapema mwaka ujao.
Presentational grey line

Je facebook ina mpango gani?

Facebook haikupendelea kuzungumzia kuhusu swala hili katikati mwa kashfa ilioikumba, lakini ililazimishwa na watu waliokuwa wakiwasiliana na New York Times.
Hadi kufikia sasa , WhatsApp, Instagram na Messenger zimekuwa zikifanya kazi kivyake na kushindana kibiashara.
Kuunganisha huduma hizo kwaa kutuma ujumbe kutarahisisha kazi ya facebook.
Haitalazimika kuunda programu mpya kama vile stories ambapo huduma zote tatu zimeongeza katika programu yake bila mafanikio ya kufurahisha.
Chapa za WhatsApp, Messenger na Instagram
Image captionWhatsApp, Messenger na Instagram ni bidhaa huru zinazoshindana
Mawasiliano ya ujumbe kupitia huduma moja hadi nyengine yanaweza kuimarisha biashara katika huduma moja kwa kutuma ujumbe kwa huduma nyengine.
Pia yatairahisishia facebook kugawana data katika huduma zote tatu ili kusaidia juhudi za matangazo yake.
Hatua hiyo pia itaimarisha uwepo wa facebook na kuwa vigumu kuanguka iwapo serikali husika zitajaribu kuivunja kwa manufaa yao ya kibinafsi.

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 28.01.2019: Giroud, Bolasie, Silva, Gueye, Crouch

Olivier Giroud

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionOlivier Giroud ana mashaka iwapo atapata muda wa kutosha wa kucheza baada ya Chelsea kumsajili Higuain.
Olivier Giroud,32, amesema anaweza kurudi kwenye ligi ya Ufaransa baada ya klabu yake ya sasa Chelsea kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Gonzalo Higuain. (Goal)
Winga wa Everton Yannick Bolaise, 29, ameiambia klabu yake kuwa anataka kutoka tena kwa mkopo baada ya kukatisha mkataba wake wa mkopo na Aston Villa. Klabu za Newcastle, Burnley na Cardiff zinammezea mate mhezaji huyo. (Mirror)
Paris St-Germain wametangaza dau la pauni milioni 21.5 kumsajili kiungo wa Everton Idrissa Gueye - lakini Everton imekataa ofa hiyo na kusema mchezaji huyo mwenye miaka 29. (Sky)
Kiungo wa Leicester Adrien Silva, 29, anataka kuondoka klabuni hapo kabla ya dirisha la usajili mwezi huu kufungwa. Silva hajawahi kupangwa kwenye kikosi cha kwanza katika Ligi ya Premia tika msimu huu ulipoanza. (Guardian)
Adrien SilvaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAdrien Silva achoshwa na kusalia benchi klabuni Leicester
Kocha mpya wa klabu ya Stoke Nathan Jones anataka kukipa nguvu mpya kikosi chake kwa kukaribisha ofa za timu zinazowataka wachezaji wake wakongwe watatu - Bojan, Darren Fletcher na Peter Crouch - ambao ndio wanaopokea malipo makubwa Zaidi klabuni hapo. (Daily Mail)
Peter CrouchHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji mkongwe Peter Crouch akalia kuti kavu klabuni Stoke.
Beki wa West Ham Reece Oxford, 20, anatakiwa na kocha Martin O'Neil wa klabu ya ligi ya daraja la kwanzaya Nottingham Forest, klabu hiyo imetenga kitita cha pauni milioni 8 ili kumnasa kinda huyo. (Mirror)
Oxford tayari ameshacheza kwa mkopo katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga, na klabu ya Eintracht Frankfurt pia wameonesha nia ya kumsajili karika dirisha la usajili la mwezi huu. (Sky)
Ben WoodburnHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBen Woodburn anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji goli mdogo zaidi katika historia ya Liverpool
Ben Woodburn, 19, ambaye ni mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga bao akiwa na umri mdogo zaidi katika historia ya Liverpool anaweza kujiunga na klabu ya Hull kwa mkopo baada ya kumaliza muda wake wa mkopo na Sheffield United. (Daily Mail)

KOCHA WA KENYA AFICHUA SIRI YA KUBEBA NDOO KATIKA ARDHI YA BONGO


KOCHA wa timu ya KK Sharks William Muluya amesema wachezaji wake walijituma muda wote Uwanjani hali iliyowafanya wakabeba ubingwa wa kombe la SportPesa Cup mwaka huu.

KK Sharks wamelitwaa kombe hilo jana baada ya Gor Mahia kuvuliwa ubingwa na kikosi cha Mbao katika hatua ya robo fainali Uwanja wa Taifa.

"Kwangu mimi naona wachezaji wamefanya kazi yao hasa ukizingatia namna ambavyo wamejitoa na kujituma muda wote Uwanjani na wameweza kupata matokeo chanya.

"Sina la kuzungumza zaidi ya kuwapongeza kwa kile ambacho wamekifanya ni hatua kubwa na ni kitu cha kujivunia kutwaa ubingwa," alisema Muliya.

Mashindano ya SportPesa Cup yamemalizika jana ambapo mshindi wa kwanza amepewa zawadi ya kombe la SportPesa Cup pamoja na dola 30,000. Pia atapata nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Everton ya England.

MBELGIJI ASHANGAZWA NA UBUTU WA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI


KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Aussems ameshangazwa na ubutu wa safu ya ushambuliaji yake ndani ya dakika 90 kwa kushindwa kufunga mabao katika mchezo wao wa jana mbele ya Mbao FC.

Simba alicheza na Mbao katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ambapo ndani ya dakika 90 hakuna timu iliyoweza kufunga licha ya kutengeneza nafasi nyingi.

Aussems amesema walipaswa wafunge mabao zaidi ya matano kutokana na nafasi walizotengeneza ila walishindwa kwa kukosa umakini uwanjani.

"Sio jambo nzuri kwangu maana wachezaji wangu wamecheza vizuri na wametengeneza nafasi nyingi wameshindwa kuzitumia hili ni tatizo kubwa ambalo natakiwa kulifanyia kazi.

"Kila mmoja ameonesha uwezo wake ndani ya kikosi ila kwa namna walivyopoteza nafasi si jambo la kufurahisha, wachezaji walishindwa kuwa na morali nzuri hali inayonifanya nianze upya kuwajenga warejee kwenye ubora wao," alisema Aussems.

Simba alishinda mchezo huo kwa penalti 5-3 na kuwafanya wawe washindi wa tatu wa mashindano hayo huku bingwa akiwa ni KK Sharks wa Kenya akifuatiwa na Bandari ambaye ni mshindi wa pili.