Sunday, 13 January 2019

SIMBA HII NI JUZI, JANA NA LEO, VIFAA VINGINE VYATUA ZANZIBAR KUONGEZA NGUVU MAPINDU


Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura jana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wachezaji watatu wa Simba wamesafiri leo kuelekea Zanzibar kuongeza makali ya Mapinduzi CUP.

Haruna Niyonzima, Rashid Juma na Shiza Kichuya ndiyo waliosafiri kuelekea visiwani humo tayari kwa fainali hiyo.

Simba ilitinga fainali baada ya kuiondoa Malindi FC kwa mikwaju ya penati ikiwa ni baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya 0-0.


No comments:

Post a Comment