Monday, 7 January 2019

MALINDI YAIONYESHA MLANGO WA KUTOKEA KOMBE LA MAPINDUZI YANGA

BAADA ya kupoteza mchezo wa leo wa kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Malindi Yanga wanayaaga mashindano rasmi.

Yanga wanaishia hatua ya makundi ya kombe la Mapinduzi baada ya kupoteza michezo yao miwili kati ya mitatu waliyocheza paka leo baada ya kufungwa na Azam FC kwa mabao 3-0 na leo na Malindi SC kwa mabao 2-1.

Mchezo wao wa mwisho utakuwa dhidi ya Jamhuri ukiwa ni kwa ajili ya kukamilisha ratiba kisha watarejea nyumbani.

Kundi B ambalo wapo kwa sasa vinara ni Azam FC wakiwa sawa na Malindi SC wenye Pointi saba wakifuatiwa na Yanga wenye Pointi tatu huku KVS wakiwa na Pointi moja kwenye kundi B.

No comments:

Post a Comment