Akizungumza kwenye maonesho ya tano ya biashara Maisara Kepteni Ramadhan Shehe kutoka kwenye shirika hilo amesema shirika linapokea kesi za upandishwa wa bei za tiketi kiholela kwa abiria wanaosafiri kwenda Dar es salamu na Pemba kitendo ambavyo linaondoa nguvu kazi ya shirika hilo.
Amesema tayari hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa kwa wanaobainika kupandisha bei kubwa za tiketi kwa abiria kwani hali hiyo itakapoachiwa itawaumiza wanancha hasa wenye vipato vya chini.
Aidha amesema bei zote za tiketi zilizowekwa kisheria zinatambulika kwa daraja la chini ambayo ni economcy ni elfu 25,kwa daraja la kati ni elfu35 na kwa VIP ni elfu 50 kwa boti za kampuni ya azam na kwa shirika la meli zanzibar bei zake kwa daraja la chini ni shilling elfu 18.
Hata hivyo amesema umewekwa ulinzi wa kutosha kwa hivyo abiria yoyote atakaeuziwa bei kubwa ya tiketi ametakiwa kutoa taarifa kwa shirika au askari wa karibu.
Akizungumzia suala zima la kuimarika kwa huduma za usafirishaji amesema shirika limepiga hatua kwani wanayo meli ya mapinduzi 2 ambayo kwa sasa inafanya kazi vizuri na kwa meli ya maendeleo ipo njiani kufanyiwa matengenezo ili kuweza kutoa huduma za usafirishaji lakini pia wanampango wa kuleta meli nyengine mpya ya abiria kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment