Wajasiriamali nchini wametakiwa kutumia Vyema Miradi ya Maendeleo inayoanzishwa na taasisi mbali mbali ili waweze kunufaika na Bidhaa zao wanazodhalisha.
Akisoma ripoti fupi kwa waandishi wa habari juu ya Utekelezaji wa Mradi wa kukuza ushirika juu ya asasi za kiraia katika midahalo ya sera na Maendeleo katika ukumbi wa ofisi ANGOZA Mombasa Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwamvuli wa asasi za kiraia ANGOZA Hassan khamis Juma amesema Mradi huo umeelekeza nguvu zao kwa wananchi hususani Wajasiriamali ili waweze kujikwamua na ugumu wa maisha.
Amesema mpaka sasa tayari wamesha anza kutoa Elimu mbalimbali juu ya upatikanaji wa soko kwa bidhaa wanazodhalisha wajasiriamali kupitia mitandao ya kijamii.
Amesema ili mradi huo uweze kufikia malengo yaliyokusudiwa ni vyema kwa Wajasiria mali kutumia vyema soko la wazi kupitia Mitandao ya kijamii ili waweze kuendana na ukuwaji wa sayansi na Teknolojia katika kuimarisha maendeleo ya Nchi.
Amesema mbali na Mradi huo kujikita katika kuwatafutia soko Wajasiriamali lakini pia Wamejikita katika kukuza uelewa kwa wananchi juu ya nishati mbadala pamoja na kuandaa kongamano la mwaka linalotarajiwa kufanyika febuari 26-27 mwaka huu ambalo litakutanisha pamoja asasi mbalimbali za kiraia zilizopo Nchini.
Akizungumzia suala la utumiaji Nishati mbadala ambayo pia inatekelezwa na mradi huo Mkurugenzi Hassan amesema jumla ya Wanachama 60 unguja na Pemba wameshapatiwa Elimu ya Nishati mbadala na tayari imeanza kuwanufaisha.
Amesema elimu hiyo imewasaidia kuepukana na gharama za matumizi ya umeme ya kawaida ambayo baadhi ya wananchi wa kipato cha chini wanashindwa kumudu gharama hizo.
Kwa upande wake Afisa Tehema kutoka Angoza Issa Mbwana amesema licha ya elimu iliyotolewa juu ya kutumia Mitandao ya kijamii kwa wajasiriamali bado mwamko umekuwa mdogo ambapo jumla ya wajasiriamali 41 waliopatiwa mafunzo 22 pekee ndio wanaoendelea kutumia mitandao kutangaza bidhaa zao.
Aidha amesema wataendelea kushirikiana na wajasiriamali mbalimbali katika kukuza bidhaa zao hususan katika masuala ya Vifungashio ,ubora na jinsi ya kupata masoko kupitia mitandao ya kijamii.
Mradi huo wa kukuza ushirika wa asasi za kiraia katika Midahalo ya kisera na maendeleo umekusudiwa kutekelezwa katika kipindi cha Miezi 11 ambapo umeanza juni 2018 na unatarajiwa kumalizika April2019 chini ya ufadhili wa Jumuiya ya ulaya EU.
No comments:
Post a Comment