Mshambuliaji wa JS Saoura, Mtanzania, Thomas Ulimwengu alijikuta kwenye wakati mgumu katika mchezo huo kutokana na kuzomewa na mashabiki wa Simba alipoingia kipindi cha pili akitokea benchi.
Licha kuzomewa na mashabiki hao, Spoti Xtra lilimshuhudia mchezaji huyo akicheka bila ya kuwajali mashabiki hao ambao walikuwa wakimzoea kabla ya kukaa kwenye benchi akitokea vyumbani.
Hali hiyo iliendelea dakika 57 kufuatia mchezaji huyo kuingia kuchukua nafasi ya Younes Koulkheir, ambapo mashabiki walilipuka kwa kelele za kumzomea Katika hatua nyingine jana Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa na Naibu Spika wa Bunge Tulia Atkson waliungana na mashabiki uwanjani hapo.
Waziri Majaliwa aliingia dakika ya 51 ambapo alishuhudia bao la pili la Simba lililofungwa na Kagere, lakini Tulia alikuwepo kuanzia mwanzoni mwa mchezo huo.
MO ASHANGILIWA
Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ aliingia uwanjani majira ya saa 9:43 alasiri na kuibua shangwe uwanja mzima kwa mashabiki kumshangilia wakiimba jina lake. Kikosi cha Simba kilikuwa hivi; Aishi Manula, Nicholaus Gyan, Mohamed Hussein Tshabalala, Juuko Murshid, Paschal Wawa, James Kotei, Hassan Dilunga/ Muzamiru Yasin, Jonas Mkude, John Bocco/ Meddie Kagere, Emmanuel Okwi/Shiza Kichuya na Clatous Chama.
No comments:
Post a Comment