Monday, 28 January 2019

MBELGIJI ASHANGAZWA NA UBUTU WA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI


KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Aussems ameshangazwa na ubutu wa safu ya ushambuliaji yake ndani ya dakika 90 kwa kushindwa kufunga mabao katika mchezo wao wa jana mbele ya Mbao FC.

Simba alicheza na Mbao katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ambapo ndani ya dakika 90 hakuna timu iliyoweza kufunga licha ya kutengeneza nafasi nyingi.

Aussems amesema walipaswa wafunge mabao zaidi ya matano kutokana na nafasi walizotengeneza ila walishindwa kwa kukosa umakini uwanjani.

"Sio jambo nzuri kwangu maana wachezaji wangu wamecheza vizuri na wametengeneza nafasi nyingi wameshindwa kuzitumia hili ni tatizo kubwa ambalo natakiwa kulifanyia kazi.

"Kila mmoja ameonesha uwezo wake ndani ya kikosi ila kwa namna walivyopoteza nafasi si jambo la kufurahisha, wachezaji walishindwa kuwa na morali nzuri hali inayonifanya nianze upya kuwajenga warejee kwenye ubora wao," alisema Aussems.

Simba alishinda mchezo huo kwa penalti 5-3 na kuwafanya wawe washindi wa tatu wa mashindano hayo huku bingwa akiwa ni KK Sharks wa Kenya akifuatiwa na Bandari ambaye ni mshindi wa pili.

No comments:

Post a Comment