Friday, 18 January 2019

Nyumba yateketea kwa moto Melinne Uzi, Serikali yatoa mkono wa pole

Akikabidhi Vifaa Hivyo Huko Kijitoupele Mkurugenzi Mtendaji Wa Kamisheni Ya Kukabiliana Na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame Amesema Wameamua Kukabidhi Msaada Kwa Familia Hiyo kwa lengo la kuhakikisha maisha yao yanarudi katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kukumbana na kadhia hiyo.
Akivitaja Vitu Walivyokabidhi Amesema Kuwa Ni Pamoja Na Mabati 30,Matofali 300,Magodoro 4,Sare Za Skuli kwaajili ya Watoto waliokuwa wakisoma ambapo kwa ujumla vitu hivyo vimefikia kiasi cha Shilingi Milioni Moja Na Laki 2.
Na Kwa Upande Wa Uongozi Wa Jimbo Umekabidhi Sh.Laki 4 Na Tanki La Maji Lenye Thamani Ya Sh.Milioni Moja Na Laki Moja Ili Kuwaondoshea Usumbufu Wanaoupata Wananchi Baada Ya Tenki Walilokuwa Wakitumia Katika Nyumba Hiyo Kuharibika Na Kusababisha Usumbufu Kwa Wananchi.
Aidha Makame Amewataka Wananchi Wanaotumia Vifaa Vya Umeme Kuchukuwa Tahadhari Ili Kujinusuru Na Madhara Yanayoweza kuepukika.
Hata Hivyo Amewataka Wananchi Kufuata Ujenzi Wa Mipango Miji Wanapojenga nyumba zao ili Kukiwezesha Kikosi Cha Zima Moto Na Uokozi Kufika Katika Maeneo yaliyokubwa na miripuko ya moto Kwa Haraka Na Kutoa Huduma Stahiki Wakati Yanapotokea Majanga Kama Hayo.
Kwa Upande Wake Mwakilishi Wa Jimbo La Kijitoupele Ali Suleiman Shihatta Ameipongeza Kamisheni Ya Kukabiliana Na Maafa Kwa Kuwafariji Wananchi Wao Na Kuwaomba Kuzidi Kutoa Elimu Kwa Jamii Ili Waweze Kujikinga Na Majanga Yanayoweza Kuepukika.
Amesema Tukio Hilo La Nyumba Kuunguwa Moto Na Kuteketeza Kila Kitu Kilichokuwemo Katika Nyumba Hiyo Kwa Madai Ya Hitilafu Za Umeme limetokea wiki chache nyuma na kuwagusa Viongozi Na Wananchi Na Kuwaomba Wahusika Kuwa Na Ustahamilivu.

No comments:

Post a Comment