Facebook ina mipango ya kuunganisha huduma zake za kutuma ujumbe katika Instagram, WhatsApp na Facebook Messenger.
Licha ya kwamba huduma zote tatu zitasalia kuwa programu huru zitashirikiana kupitia ujumbe utakaotumwa kutoka huduma moja hadi nyingine.
Facebook imeambia BBC kwamba ndio mwanzo wa mchakato mrefu.
- Watu wawili wajeruhiwa katika mlipuko wa bomu Nairobi
- Kucheka na watu ni muhimu mara 30 zaidi
- Kwa picha, mkasa wa bwawa Brazil
Mpango huo kwanza uliripotiwa mjini New York na unaaminika kuwa mradi wa kibinafsi wa mwanzilishi wa facebook Mark Zuckerberg.
Utakapokamilika , ushirikiano huo utamaanisha kwamba mtumiaji wa facebook anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtu ambaye anamiliki akaunti ya WhatsApp.
Hili haliwezekani kwa sasa kwa kuwa programu zilizopo hazina uhusiano.
Hatua ya kuunganisha huduma hizo tatu umeanza , kulingana na gazeti la The new York Times na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019 ama mapema mwaka ujao.
![Presentational grey line](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/media/images/74982000/jpg/_74982321_line976.jpg)
Je facebook ina mpango gani?
Facebook haikupendelea kuzungumzia kuhusu swala hili katikati mwa kashfa ilioikumba, lakini ililazimishwa na watu waliokuwa wakiwasiliana na New York Times.
Hadi kufikia sasa , WhatsApp, Instagram na Messenger zimekuwa zikifanya kazi kivyake na kushindana kibiashara.
Kuunganisha huduma hizo kwaa kutuma ujumbe kutarahisisha kazi ya facebook.
Haitalazimika kuunda programu mpya kama vile stories ambapo huduma zote tatu zimeongeza katika programu yake bila mafanikio ya kufurahisha.
![Chapa za WhatsApp, Messenger na Instagram](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/15F6B/production/_105336998_fb-nc.png)
Mawasiliano ya ujumbe kupitia huduma moja hadi nyengine yanaweza kuimarisha biashara katika huduma moja kwa kutuma ujumbe kwa huduma nyengine.
Pia yatairahisishia facebook kugawana data katika huduma zote tatu ili kusaidia juhudi za matangazo yake.
Hatua hiyo pia itaimarisha uwepo wa facebook na kuwa vigumu kuanguka iwapo serikali husika zitajaribu kuivunja kwa manufaa yao ya kibinafsi.
No comments:
Post a Comment