Wednesday, 9 January 2019

TIBOROHA AAHIDI MAKUBWA YANGA, AZINDUA KAMPENI RASMI LEO


Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha,  hatimaye leo amezindua rasmi kampeni zake za kuwania nafasi ya mwenyekiti katika klabu hiyo.

Katika uzinduzi huo uliyofanyikia makao makuu ya klabu hiyo amewatambulisha baadhi ya wajumbe wanane atakaoambatana nao, ambao ni Ally Msigwa, Christopher Kashililika, Dominic Francis na Salim Rupia.

Wengine ni Arfat Hadji, Said Barala na Peter Simon ambao wote ni wagombea katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.

Tiboroha ameanika vipaumbele vyake kuwa akipewa ridhaa ataanza na kujenga na kuimarisha taasisi hiyo,  pili atafanya juhudi za haraka kuirudisha klabu kwa wanachama na mashabiki wake.

Pia amesema  atafanya kazi ya kuimarisha matawi, atajenga mara moja misingi ya uwekezaji na biashara, kuimarisha na kujenga mifumo ya klabu na kushirikisha wadau wote.

No comments:

Post a Comment