Tuesday, 29 January 2019

CAF yasogeza mbele mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamua kusogeza mbele kwa wiki moja kuanza kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika 2019, kutoka Juni 14 hadi Juni 21 kwa sababu ya kupisha mfungo wa radamani.
Makamu wa rais wa Shirikisho la Soka la Misri (EFA), Ahmed Shobir alitangaza kuwa CAF wamefikia uamuzi huo baada ya kupata maombi kutoka nchi mbalimbali.
“Nchi za Afrika Kaskazini zimeomba CAF kusongeza mbele kwa wiki moja kufanyika kwa mashindano hayo ili kutoa nafasi ya kumalizika mfungo wa Ramadan pamoja na kusherekea siku kuu ya Eid Al-Fitr,” alisema Shobir.
“CAF imekubaliana na nchi kuhusu kusogeza mbele tarehe ya kuanza mashindano kuwa Juni 21 badala ya Juni 14, hivyo mashindano haya yatafikia mwisho Julai 19, 2019,” aliongeza Shobir.
Novemba, CAF ilipoka wenyeji Cameroon kutokana na kuchelewa kukamilisha maandalizi ya miji yake kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 24.
Misri wamechukua wenyeji wa AFCON baada ya  Morocco iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kuchukua wenyeji huo, lakini dakika za mwisho walijitoa.
Misri ilipata kura 16 kati 18 zilizopigwa na wajumbe wa CAF, huku kura moja ikienda kwa Afrika Kusini katika mchakato wa kupata mwenyeji mpya.
Hii ni mara ya tano kwa Misri kuwa wenyeji wa AFCON baada ya kufanya hivyo 1959, 1974, 1986 na 2006, huku Mafarao hao wakishinda mara tatu kati ya mara nne walizokuwa wenyeji.

No comments:

Post a Comment