Monday, 21 January 2019

YANGA SASA MAMBO NI MOTO, KIFAA KILICHOKUWA NJE YA NCHI KWA MUDA CHAREJEA


Baada ya kukosekana nchini na dimbani akiitumika klabu yake kwa mechi kadhaa, kiungo mkongomani wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi ametua rasmi nchini.

Tshishimbi ambaye alisafiri kwao kwenda kutatua matatizo kadhaa ya kifamilia kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa mabosi wake, amerejea na leo amehusika katik mazoezini ya asubuhi.


Kiungo huyo fundi bado hajaonesha cheche zake msimu huu baada ya miezi kadhaa nyuma kuwa sehemu ya wachezaji walio majeruhi Yanga.

Hivi sasa kikosi kipo katika maandalizi ya SportPesa Super CUP ambayo itafanyika hapa nchini.

Tayari Tshishimbi ameshaungana na wenzake kambini na kuna uwezekano mkubwa akawa mmoja wa watakocheza mashindano hayo ambayo yanakuwa chini ya udhamini wa kampuni hiyo ya bahati nasibu.

No comments:

Post a Comment